Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kiburi ni janga katika safari ya kiroho. Kwa maneno yenye mwanga kutoka kwa Ayatollah Haairi Shirazi (rahimahu Allah), tujifunze jinsi ya kujiepusha na tabia ya kujiona bora.
Msafiri anayesafiri kuelekea kwenye lengo, huona njia ambayo bado haijapitiwa mbele yake; lakini akiigeuzia kisogo safari, ataona njia ambayo tayari imepitwa.
Yule anae yaona aliyo yafanya na aliyo yapitia, ni lazima aamini kuwa yupo katika makosa na lengo lake ameligeuzia kisogo; na yule anae yaona ambayo hayaja fanywa na yaliyo mbele yake, asiwe na shaka kuwa amesimama kuielekea safari na yupo katika njia sahihi.
Basi, ikiwa kiburi au kujivuna kunajitokeza kidogo tu katika matendo ya mtu, hiyo ni alama kuwa anashuka chini na anaporomoka. Mtu wa aina hii anatakiwa amkimbilie Mwenyezi Mungu na aelekeze fikra zake kwenye yale mambo ambayo bado hajayafanya, ili asije akaingia katika kiburi.
Chanzo: "Tamthilat Akhl'aq", juzuu ya kwanza, uk, 40.
Maoni yako